Friday, June 7, 2013

DIAMOND NA PENNY YASEMEKANA HIVI KARIBUNI KUWA WAZAZI

Na Imelda Mtema
TUMEINYAKA kwamba mimba anayotamba staa wa Bongo Fleva, Nasibu Abdul ‘Diamond Platnumz’ kuwa amempachika mpenzi wake, Peniel Mungilwa ‘Penny’, inadaiwa kuanza kumtesa mtangazaji huyo wa DTV, Ijumaa Wikienda linashuka nayo.
Penny akiwa hospitali.
Habari zisizokuwa na chenga kutoka kwa chanzo chetu ambacho ni mtu wa karibu wa mrembo huyo, zilieleza kwamba kufuatia hali hiyo, Penny alikimbizwa kwenye Hospitali ya Regency, Dar wikiendi iliyopita kisha  akalazwa, akachomwa sindano na kutundikiwa dripu.

Diamond na Penny katika pozi.
Akizungumzia hali hiyo, Penny aliliambia gazeti hili kuwa ni kweli alizidiwa usiku na alikimbizwa hospitali ambapo pamoja na mengine lakini kubwa vipimo vilionesha kuwa alikuwa na malaria.
Hata hivyo, habari tulizozipata wakati tunakwenda mitamboni zilieleza kuwa Penny aliruhusiwa kutoka hospitalini na anaendelea vizuri.

Thursday, June 6, 2013

AMANDA AFUNGUKA,SIKIA.....

Na Gladness Mallya
MWIGIZAJI, Tamrina Poshi ‘Amanda’ amefunguka kuwa Wabongo wengi wamekuwa hawana elimu ya masuala ya misiba kwa kutolea mfano kifo cha msanii, Albert Mangwea ‘Ngwair’.
Albert Mangwea ‘Ngwair’.
Akifafanua kauli yake, Amanda alianza kwa kuwapaka wote ambao walikuwa wakim-tag picha za marehemu Mangwea kwenye mtandao wa Facebook ambazo kimsingi alidai si busara kimaadili ya mwafrika na kuwataka waache mara moja.
“Siyo vyema kusambaza picha za marehemu tena za mochwari, vuta picha kama ingekuwa ndugu yako ungefanya hivyo? Naombeni muache hiyo tabia na mjifunze kuanzia sasa,” alisema Amanda.

BINTI WA MICHAEL JACKSON,ATAKA KUJIUA

                                      Paris Michael Jackson anayesemekana alitaka kujiua.
PARIS, binti wa aliyekuwa mwanamuziki maarufu wa Marekani, hayati  Michael Jackson, amelazwa hospitali baada ya kunusurika kujiua ikiwa ni siku chake kabla ya kutimia miaka minne ya kifo cha baba yake. Binti huyo ana umri wa miaka 15.
Binti huyo aliyelazwa hospitalini mjini Los Angeles anasemekana alimeza madawa kuliko kiwango kinachotakiwa.
Kwa mujibu wa Perry Sanders ambaye ni mwanasheria wa mama yake hayati Michael (Katherine Jackson), msichana huyo alichukuliwa na gari la wagonjwa saa 7.27 usiku na kupelekwa hospitali ambako hali yake inaendelea vyema.…
                                      Paris Michael Jackson anayesemekana alitaka kujiua.
PARIS, binti wa aliyekuwa mwanamuziki maarufu wa Marekani, hayati  Michael Jackson, amelazwa hospitali baada ya kunusurika kujiua ikiwa ni siku chake kabla ya kutimia miaka minne ya kifo cha baba yake. Binti huyo ana umri wa miaka 15.
Binti huyo aliyelazwa hospitalini mjini Los Angeles anasemekana alimeza madawa kuliko kiwango kinachotakiwa.
Kwa mujibu wa Perry Sanders ambaye ni mwanasheria wa mama yake hayati Michael (Katherine Jackson), msichana huyo alichukuliwa na gari la wagonjwa saa 7.27 usiku na kupelekwa hospitali ambako hali yake inaendelea vyema.
Mwanasheria huyo pia hakutaka kuelezea sababu iliyomfikisha msichana huyo hospitali isipokuwa aliishia kusema tu kwamba hali yake inaendelea vizuri.
                                                           (Chanzo: The Independent)                                      Paris Michael Jackson anayesemekana alitaka kujiua.

PARIS, binti wa aliyekuwa mwanamuziki maarufu wa Marekani, hayati  Michael Jackson, amelazwa hospitali baada ya kunusurika kujiua ikiwa ni siku chake kabla ya kutimia miaka minne ya kifo cha baba yake. Binti huyo ana umri wa miaka 15.
Binti huyo aliyelazwa hospitalini mjini Los Angeles anasemekana alimeza madawa kuliko kiwango kinachotakiwa.
Kwa mujibu wa Perry Sanders ambaye ni mwanasheria wa mama yake hayati Michael (Katherine Jackson), msichana huyo alichukuliwa na gari la wagonjwa saa 7.27 usiku na kupelekwa hospitali ambako hali yake inaendelea vyema.
Mwanasheria huyo pia hakutaka kuelezea sababu iliyomfikisha msichana huyo hospitali isipokuwa aliishia kusema tu kwamba hali yake inaendelea vizuri.
 
JANA BBA,WATZ TUMEFIKA SIKU YA 10

Mshiriki anayeiwakilisha Tanzania Feza Kessy katika pozi.
Mshiriki mwingine kutoka Tanzania Ammy nando

MWILI WA MALEHEMU NGWEA WAPIGWA STOP PANDE ZA MIKESE

Wataka kujua nini kilitokea soma hapa,
 Wanamchi wa maeneo ya mikese, wamekusanyika na kuusimamisha msafara uliobeba mwili wa marehem Ngwea kwa kutaka na wao wamuage, akizungumza na Cloud Fm "Moe Fire" amesema walikutana na kundi la watu na kudhani labda kuna tatizo. Baada ya kusimamishwa na trafic na kuuliza tatizo ni nini, Trafic alisema kuwa wananchi hao wamekusanyika na ili kuuaga mwili wa marehem Ngwea na kudai kitendo hicho kikifanyika ndio amani itapatikana.
Kilichofanyika ni kuruhusu watu wle walishike gari lililokuwa na mwili wa Ngwea na kuondoka, lakini baada ya kuondoka, zaidi ya pikipiki 50 walizozikuta pale ziliongoza msafara huku magari mengine pia yakiunga msafara huo.

MWIMBAJI WA MIONDOKO YA TAARABU KHADIJA KOPA AFIWA NA MUMEWE

HABARI
Malkia wa mipasho Khadija Omari Kopa amefiwa na mumewe (Jaffari Ally) usiku wa kuamkia leo katika hospitali ya Lugalo, jijini Dar es salaam.Marehem alilazwa katika hospitali hiyo siku ya jumatatu ya wiki hii, na mpaka anafariki mke wake (Kadija Kopa) alikuwa Rukwa kikazi ambapo leo hii anatarajiwa kufika jijini Dar kwa ajili ya mazishi ya mumewe. msiba kwa Dar upo maeneo ya mtogole nyumbani kwa mama yake marehem Jaffari