Thursday, June 6, 2013

AMANDA AFUNGUKA,SIKIA.....


Na Gladness Mallya
MWIGIZAJI, Tamrina Poshi ‘Amanda’ amefunguka kuwa Wabongo wengi wamekuwa hawana elimu ya masuala ya misiba kwa kutolea mfano kifo cha msanii, Albert Mangwea ‘Ngwair’.
Albert Mangwea ‘Ngwair’.
Akifafanua kauli yake, Amanda alianza kwa kuwapaka wote ambao walikuwa wakim-tag picha za marehemu Mangwea kwenye mtandao wa Facebook ambazo kimsingi alidai si busara kimaadili ya mwafrika na kuwataka waache mara moja.
“Siyo vyema kusambaza picha za marehemu tena za mochwari, vuta picha kama ingekuwa ndugu yako ungefanya hivyo? Naombeni muache hiyo tabia na mjifunze kuanzia sasa,” alisema Amanda.

No comments:

Post a Comment