Wednesday, May 29, 2013

je, UNAJUA IZI INFOR.....

HUYU NDO BABA MZAZI WA WEMA SEPETU

 SIKU CHACHE kupitia mtandao wa Instagram, Pttiman alitupia picha akiwa baba yake mzazi, mzee Sepetu, huku pembeni akiwepo mtu wake wa karibu sana "Pettiman. Nimeona ni vizuri kushare na wewe, kwasababu nilikuwa sijawahi kabisa kumuona sehem yoyote

MASO GANGE TENAAAAAAAA.

VIDEO Queen wa Bongo Fleva, Agness Jerald ‘Masogange’ anasumbuliwa na tatizo la kuota ndoto mbaya usiku na kuamka kisha kutoka nje na kutimua mbio, jambo ambalo kwa wengi linaweza kuonekana kuwa ni maajabu.

Habari kutoka kwa sosi wangu, zinasema kuwa katikati ya wiki iliyopita, Masogange akiwa ndotoni, aliamka na kufungua milango na geti la nje kisha kutimua mbio umbali mrefu akiwa na nguo za kulalia na miguuni hana  viatu.
“Bahati nzuri ni kwamba, wakati…
Agness Jerald ‘Masogange’.
Habari kutoka kwa kitaa, zinasema kuwa katikati ya wiki iliyopita, Masogange akiwa ndotoni, aliamka na kufungua milango na geti la nje kisha kutimua mbio umbali mrefu akiwa na nguo za kulalia na miguuni hana  viatu.
“Bahati nzuri ni kwamba, wakati anahangaika kufungua geti, rafiki yake aliyekuwa amelala naye alishtuka na kushangaa kukuta milango iko wazi. Alipotoka nje, akakuta Masogange ndiyo anamalizia kufungua geti kubwa na kuanza kukimbia hivyo akamkimbiza,” kilieleza chanzo chetu.
Akaongeza: “Lakini pia aliwapigia simu marafiki zake wengine na kuwajulisha juu ya tukio hilo, maana mwenyewe ilikuwa mara ya kwanza kumuona katika hali hiyo.”
MASOGANGE ANASEMAJE?
Risasi Mchanganyiko kama ilivyo kawaida yake ya kutokukurupuka, lilimsaka Masogange kwa simu na kufanikiwa ambapo alithibitisha tukio hilo na kufafanua kwamba liliwahi kumtesa kwa muda mrefu huko nyuma, likaisha.
“Ilikuwa hatari sana lakini namshukuru rafiki yangu kwa kunisaidia. Unajua hili tatizo liliwahi kunitesa sana wakati nikiwa mdogo lakini nilikwenda Mbeya nikapewa dawa tatizo likapotea kabisa hadi juzi liliporudi tena,” alisema.


TOTO LA DAR KULEEEE MBAGALA.......Duhhhh si kafunguka..unataka kujua nini?

KWA mara ya kwanza nyota wa Bongo Fleva, Nasibu Abdul 'Diamond' ameacha gumzo London, Uingereza baada ya kueleza sababu za kwa nini ni kiwembe?
Diamond akiwa na Penny. Akifunguka katika mahojiano maalum wiki iliyopita na Kipindi cha Sporah Show cha runingani alipokuwa kwenye ziara ya kimuziki nchini humo, Diamond alizungumza ishu kibao za kimapenzi hasa juu ya msururu wa wanawake ambao tayari ametoka nao.
ASISITIZA ANASUBIRI MTOTO
Kabla ya yote, staa huyo alisisitiza kuwa muda si mrefu anatarajia kupata mtoto kutoka kwa mpenzi wake wa sasa, Peniel Mungilwa ‘Penny’ akimaanisha kuwa ni mjamzito, kinyume na msichana huyo ambaye hivi karibuni alimshangaa Diamond kueneza habari hizo.


...akiwa na Wema. KWA NINI ANAPENDA KUBADILISHA WANAWAKE?
Diamond: Mimi ni binadamu kama binadamu wengine wa kawaida. Nampenda mwanamke anayenipenda na kuniheshimu. Ikitokea mikwaruzano huwa mimi nakaa pembeni, natafuta sehemu nyingine. Wakati mwingine mimi ndiye huwa naachwa.
KWA NINI MSURURU NDANI YA KIPINDI CHA MIAKA MITATU?
Diamond: Nikiwa na mtu nikiachana naye naonekana nina matatizo kwa sababu wakati mwingine nakuwa na wanawake wenye majina. Siwezi kukaa bila uhusiano na nakuwa wazi kwa sababu lazima itajulikana tu na kuandikwa kwenye magazeti. Kuna kipindi nilikaa miezi sita bila kufanya kitu chochote (mh!). Lakini nikianza (uhusiano), nikihama naonekana msumbufu.

...akiwa na Jokate.
KWA NINI MASTAA, TENA MARAFIKI?
Diamond: Huwa sitoki, nakuwa nyumbani tu, nakaa na mama yangu (Sanura Kassim ‘Sandra’) nampikia. Nikitoka nakwenda kwenye shoo au studio. Huko ndiko nakutana nao (mastaa wa kike).
ALIMPATAJE JOKATE (MWEGELO)?
Diamond: Alikuwa anazindua nguo zake (Kidoti) akaniomba nikapite nazo kwenye onesho la mavazi, nikapita nazo jukwaani. Baada ya hapo na mimi nilimuomba nifanye naye video ya wimbo wangu (Mawazo), ndiyo ikatokea kama hivyo.
NINI KILIMVUTIA KWA PENNY?
Diamond: Kwanza mimi nilimjua Penny kabla ya Wema (Sepetu), alikuwa mshikaji wangu. Ni mwanamke mzuri, wa kileo, ana akili adabu na heshima. Anampenda mama yangu na familia yangu ‘coz’ na mimi nampenda mama yangu (sifa ambazo kwa mujibu wake Wema alizikosa).
KWA NINI ALIMREKODI WEMA?
Diamond: Kila binadamu anajiona yupo sawa na anaonewa. Sipendi kuongea, nitazungumza vibaya. Mapenzi yanaumiza na mimi naumia pia lakini watu wanadhani mimi ndiye muumizaji. Unamwambia mtu kwa nini una mwanaume mwingine.
Anakuzuga sijui ni pedeshee anampa pesa. Mara unamwona na mwanaume mwingine. Mimi siyo maskini lakini sasa mara unamwona na brazameni mwingine ‘then’ washkaji wanakwambia. Wewe unajifanya kuziba masikio mara unasikia ana mwanaume mwingine. Lakini ikafika wakati nikajikuta naumia sana kwenye mapenzi.


...akiwa na Jokate. Kama ukisikiliza ule wimbo wa Kesho ni kweli kabisa. Mimi nikakaa pembeni hadi nilipompata huyu wa sasa (Penny).
Nakumbuka (Wema) alinipigia simu akadai mimi ndiye nasema anataka turudiane. Nilikuwa kwenye gari, nikamuuliza anataka nini?
Wakati huo nilishafika nyumbani kwa baby wangu. Nikamwonesha ona sasa, anasema mimi ndiyo nataka nirudiane naye, anatangazia watu hadi saluni kuwa nataka kurudiana naye na kujidai kwenye vyombo vya habari kuwa ananipenda. Kumbe ana wengine (ving’asti) kama ishirini anawahonga (mistari ya wimbo wake wa Nataka Kulewa).
Nilimpa baby wangu akamwambia kistaarabu tuache tulale. Sasa kuna mtu wetu wa karibu ndiye aliyehusika kusambaza ile sauti.
SEMA UKWELI, ULILALA NA UWOYA?
Diamond: (kicheko) Ningeanzia wapi? Unajua mimi ni simba kwa hiyo nikionekana na swala inajulikana lazima nimle hata kama tumeenda sehemu tu kuzungumza ishu za kazi.
KWA NINI WANAWAKE AU ENZI ZILE HAKUWA NA ‘CHANSI’ SASA AMEPATA?
Diamond: Ukimuelimisha mwanamke mmoja umeelimisha ulimwengu mzima. Nawapenda sana, wanajaa tele kwenye shoo zangu. Kilichotokea kwa Wema ilibidi tu sikuwa na jinsi.
ANATAKA MWANAMKE WA AINA GANI?
Diamond: Ukimuuliza mwanamke aliyewahi kuwa na mimi atakwambia najua mapenzi, najua kupetipeti, najua kubembeleza, najua kujifanya mjinga. Narudia tena, awe mzuri, wa kileo, mwenye akili, anayejiheshimu, ampende mama yangu kama mimi ninavyompenda mama yangu.

Nasibu Abdul 'Diamond'.
KWA NINI KIWEMBE?
Uchunguzi uliofanywa na Ijumaa ulibaini kuwa chanzo cha staa huyo aliyetokea Tandale, Dar kuitwa kiwembe ni kutokana na tabia yake ya kubadilisha wanawake kama nguo.
Baadhi ya aliowahi kuripotiwa akidaiwa kutoka nao ni Rehema Fabian (Miss Kiswahili 2009), Jacqueline Wolper (msanii wa filamu), Upendo Moshi ‘Pendo’ (Mshiriki wa Maisha Plus) na  Natasha (Video Queen wa Bongo Fleva).
Wengine ni Wema (mwigizaji), Jokate (mwigizaji), Aunt Ezekiel (mwigizaji), Najma (msanii wa Bongo Fleva), Penny (mtangazaji DTV), Irene Uwoya (mwigizaji) na wengineo.


KIDOTI IS GOING HOT,Waaaaaaapi NI HUKO KWAO RUVUMA

MLIMBWENDE aliyejitosa kwenye tasnia ya filamu za Kibongo na kufanya vizuri, Jokate Mwegelo ‘Kidoti’ ameanzisha Kipindi cha Kidoti Time ambacho kitafundishwa katika shule za Msingi 27 Songea vijijni Mkoani Ruvuma.…

news MPYAAAAAAA

WALE wasanii wawili waliodumu kwenye uchumba kwa muda mrefu, Ramadhan Baba ‘H.Baba’ na Flora Mvungi wameamua kuvunja ukimya na kutangaza rasmi kuwa wanatarajia kufunga ndoa Juni 8, mwaka huu.…

Tuesday, May 28, 2013

SIKU chache baada ya wasanii wa filamu Bongo, Jacqueline Wolper na Baby Madaha kuingia kwenye mzozo wa kugombea nyumba moja ya kupanga ambayo wote waliilipia kodi kwa nyakati tofauti, bifu zito linalotajwa kuwa ni la kifo limeibuka.

Jacqueline Wolper. Sakata la wawili hao lilifika polisi na kubainika kuwa Madaha alilipa kodi kwa tapeli wakati Wolper alitoa fedha zake kwa mwenye nyumba hivyo kumfanya awe na haki ya kuhamia.
Akizungumza na Ijumaa, juzi jijini Dar es Salaam, Madaha alisema pamoja na kubainika kuwa alitapeliwa, mtu pekee ambaye angeweza kumsaidia kupata fedha zake (shilingi milioni tatu) ni Wolper lakini anamchenga.
MADAI YA MADAHA
“Ni kweli nimetapeliwa lakini Wolper kama msanii mwenzangu alikuwa na uwezo wa kunisaidia maana yeye anaishi pale lakini nimemwambia, ananipiga chenga. Sitaongea naye milele, hana utu kabisa. Milioni tatu ndugu yangu si pesa ndogo.”


Baby Madaha. HUYU HAPA WOLPER
Wolper alipotafutwa na Ijumaa na kusomewa malalamiko ya Madaha alisema: “Naweza kusema Madaha hana akili, ni mpuuzi kwa sababu angekuja kwa busara nyumbani kwangu tungezungumza na baba mwenye nyumba tukajua namna ya kumsaidia.
“Lakini yeye kabla hajaomba ushirikiano kwangu, tayari naanza kusumbuliwa na magazeti kuwa eti nimemtapeli. Halafu hajawahi kunipigia simu bali alikuwa anawatuma watu wake kwangu. Kwa nini asingekuja mwenyewe?
“Ina maana yeye ni staa sana au? Huyu hana lolote anataka kupanda kwa kutumia jina langu,” alisema Wolper. 

AKA Mimi Alimaaharufu NGWEA Afariki Dunia.

Rapper, Freestyler, Ngwea amefariki dunia leo hii katika hospitali ya St Hellen iliyoko South Africa, sababu za kifo chake hazijatajwa...endelea kutembelea blog hii kwa habari zaidi.

Monday, May 27, 2013

Fashion and Beauty.


Biggie's Daughter Launches Notoriouss Clothing Line

T'yanna is releasing T-shirts with Banksy-inspired images.

Fashion and Beauty


Michelle Obama Loves Her Tracy Feith Dress

She wears this floral frock for the seventh time.

KNOW ABOUT THIS

Teen Dating Violence: What You Need to Know

Why You Have to Take Violence Seriously
of 108Photo
  • The Consequences of Abuse
  • Violence, Coerced Sex and Condoms
  • Why You Have to Take Violence Seriously
  • Know The Warning Signs
  • Dating Violence and The LGBT Community
  • When Love Hurts
  • What Is Teen Dating Violence?
  • General Dating Violence Stats
  • Blacks and Teen Dating Violence
  • What Encourages This Type of Violence?
  • The Consequences of Abuse
  • Violence, Coerced Sex and Condoms
  • Why You Have to Take Violence Seriously
  • Know The Warning Signs
  • Dating Violence and The LGBT Community
  • When Love Hurts
  • What Is Teen Dating Violence?
  • General Dating Violence Stats
  • Blacks and Teen Dating Violence
  • What Encourages This Type of Violence?
Why You Have to Take Violence Seriously

While some of the public response to Chris Brown and Rihanna’s abusive relationship from young people was alarming, it’s important to understand that violence is serious and that victims do not deserve it. Abuse is not a consequence of you doing something wrong. Read more about the dangers and consequences of teen dating violence here.


WASHILIKI WETU BBA, Big Bro in Africa

Hawaapa.......,,,
Big Brother Africa  2013 "The Chase" imeanza kwa kasi usiku wa leo (26 may) na msanii Feza Kessy na Nando ndio wanaoiwakilisha Tanzania. kwa mujibhu wa story yake mwenyewe Nando ni mtanzania anaeishi marekani lakini ilimbidi aombe hela kwa marafiki zake kwa ajili ya kupata ticket ya kuja Tanzania kufanya usahili wa BBA, amesema kama angekosa nafasi ya kuiwakilisha Tanzania asinge juta maana pia alikua hajamuona bibi yake kwa miaka mingi, kwahiyo angekuwa kaitumia nafasi hiyo kuja kumuona bibi yake.

Sunday, May 26, 2013

We thanks mama- P’ Square

Ibada ni nguzo yetu ,mama alituambia
Wasanii hao waliweka wazi hilo kwenye mahojiano maalumu kuwa,pamoja na kuwa nao kwenye kila hatua ya maisha yao lakini kitu kikubwa alichowaachia kama urithi ni kumuabudu mungu bila kuchoka.
Wanamuziki mapacha  Peter na Paul Okoye,wanaounda kundi la P’Squre,wameweka wazi kuwa pamoja na kufanya muziki wao ni waumini wazuri wa dini ya kikikristo kitu pekee ambacho wamerithishwa na marehemu mama yao.
Wasanii hao waliweka wazi hilo kwenye mahojiano maalumu kuwa,pamoja na kuwa nao kwenye kila hatua ya maisha yao lakini kitu kikubwa alichowaachia kama urithi ni kumuabudu mungu bila kuchoka.
“Mama yetu alikuwa ni mcha Mungu na mhubiri mzuri kwenye kanisa lake na siku zote alitulea katika maadili hayo mema na huo unabaki kuwa ni urthi wa pekee kwetu,”walisema pacha hao.
Aidha, Paul aliweka wazi wanakuwa baba bora kwa watoto wao kutokana na kupata malezi mazuri na yenye upendo kutoka kwa mama yao. Mama yao alifariki dunia Julai 12, mwaka jana.