Habari kutoka kwa sosi wangu, zinasema kuwa katikati ya wiki iliyopita, Masogange akiwa ndotoni, aliamka na kufungua milango na geti la nje kisha kutimua mbio umbali mrefu akiwa na nguo za kulalia na miguuni hana viatu.
“Bahati nzuri ni kwamba, wakati…
Agness Jerald ‘Masogange’.
Habari kutoka kwa kitaa, zinasema kuwa katikati ya wiki
iliyopita, Masogange akiwa ndotoni, aliamka na kufungua milango na geti
la nje kisha kutimua mbio umbali mrefu akiwa na nguo za kulalia na
miguuni hana viatu.“Bahati nzuri ni kwamba, wakati anahangaika kufungua geti, rafiki yake aliyekuwa amelala naye alishtuka na kushangaa kukuta milango iko wazi. Alipotoka nje, akakuta Masogange ndiyo anamalizia kufungua geti kubwa na kuanza kukimbia hivyo akamkimbiza,” kilieleza chanzo chetu.
Akaongeza: “Lakini pia aliwapigia simu marafiki zake wengine na kuwajulisha juu ya tukio hilo, maana mwenyewe ilikuwa mara ya kwanza kumuona katika hali hiyo.”
MASOGANGE ANASEMAJE?
Risasi Mchanganyiko kama ilivyo kawaida yake ya kutokukurupuka, lilimsaka Masogange kwa simu na kufanikiwa ambapo alithibitisha tukio hilo na kufafanua kwamba liliwahi kumtesa kwa muda mrefu huko nyuma, likaisha.
“Ilikuwa hatari sana lakini namshukuru rafiki yangu kwa kunisaidia. Unajua hili tatizo liliwahi kunitesa sana wakati nikiwa mdogo lakini nilikwenda Mbeya nikapewa dawa tatizo likapotea kabisa hadi juzi liliporudi tena,” alisema.
No comments:
Post a Comment