SIKU chache baada ya wasanii wa filamu Bongo, Jacqueline Wolper na Baby
Madaha kuingia kwenye mzozo wa kugombea nyumba moja ya kupanga ambayo
wote waliilipia kodi kwa nyakati tofauti, bifu zito linalotajwa kuwa ni
la kifo limeibuka.
Jacqueline Wolper.
Sakata la wawili hao lilifika polisi na kubainika kuwa Madaha alilipa
kodi kwa tapeli wakati Wolper alitoa fedha zake kwa mwenye nyumba hivyo
kumfanya awe na haki ya kuhamia.
Akizungumza na Ijumaa, juzi jijini
Dar es Salaam, Madaha alisema pamoja na kubainika kuwa alitapeliwa, mtu
pekee ambaye angeweza kumsaidia kupata fedha zake (shilingi milioni
tatu) ni Wolper lakini anamchenga.
MADAI YA MADAHA
“Ni kweli nimetapeliwa lakini Wolper kama msanii
mwenzangu alikuwa na uwezo wa kunisaidia maana yeye anaishi pale lakini
nimemwambia, ananipiga chenga. Sitaongea naye milele, hana utu kabisa.
Milioni tatu ndugu yangu si pesa ndogo.”
Baby Madaha.
HUYU HAPA WOLPER
Wolper alipotafutwa na Ijumaa na kusomewa
malalamiko ya Madaha alisema: “Naweza kusema Madaha hana akili, ni
mpuuzi kwa sababu angekuja kwa busara nyumbani kwangu tungezungumza na
baba mwenye nyumba tukajua namna ya kumsaidia.
“Lakini yeye kabla
hajaomba ushirikiano kwangu, tayari naanza kusumbuliwa na magazeti kuwa
eti nimemtapeli. Halafu hajawahi kunipigia simu bali alikuwa anawatuma
watu wake kwangu. Kwa nini asingekuja mwenyewe?
“Ina maana yeye ni staa sana au? Huyu hana lolote anataka kupanda kwa kutumia jina langu,” alisema Wolper.
No comments:
Post a Comment